Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masfa mafupi, limesema jeshi la Korea Kusini.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Sino-ri lililopo Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa Pyongyang.
Hatua hiyo inakuja wakati balozi wa Marekani anaehudumu huko Korea kazkazini Steve Beigun anazuru Korea kusini kutafuta vipi mazungumzo hayo yanaweza kuanzishwa upya.
Wachambuzi wanatafsiri kitendo hicho ni kutokana na kutoridhika kwa utawala wa Pyongyang na kuvunjika kwa mwendelezo wa mazungumzo yao na Marekani yaliyokuwa yafanyike mwezi February huko mjinii Hanoi.
Mwezi uliyopita Korea Kaskazini ilisema kuwa imefanyia majaribio silaha yenye kombora kali , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Kim Jong un kugonga mwamba.
Tunafahamu nini kuhusu hatua hiyo?
Makombora mawili ya masafa mafupi yalirushwasaa kumi unusu skwa saa za huko, ilisema taarifa ya pamoja ya wakuu wa kijeshi kutoka taifa jirani la Korea Kusini.
Uchunguzi wa kina unafanywa kwa ushirikiano na maafisa wa upelelezi wa Marekani, iliongeza taarifa hiyo.
Rais wa Korea kusini Moon Jae-in amemuonya kiongozi wa Korea kaskazini kutoondelea na tabia yake ya kufanya majaribio ya kufyatua makombora.
Amesema kwamba hatua hiyo itatetelesha uhusiano wao na Marekani na vilevile utawala huo wa Seoul.
Mzozo wa nyuklia unatokana na nini?
Hali ya taharuki imezuka kati ya Korea kaskazini na Marekani baada ya Washington kusisitiza kuwa Pyongyang ikomeshe mpango wake wa nyuklia.
Kiongozi wa Korea kazkazini Kim Jong-un anataka vikwazo dhidi ya nchi yake viondolewe na mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea kusini yasitishwe.
Jumamosi iliyopita Korea Kaskazini ilithibitisha kuwa rais Kim Jong-un ameongoza mwenyewe shughuli ya kufanyia majaribio makombora kadhaa ya masafa ya kadri na yale ya masafa ya mbali.
"Makombora kadhaa ya masafa mafupi" pia yalirushwa kutoka rasi ya Hodo hadi bahari ya Japan.
Mwaka uliopita , kiongozi huyo wa Korea alisema kuwa atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia na kwamba hatofanyia majaribio makombora ya masafa marefu huku uwezo wa Kinyuklia wa Pyonyang ukibainika.
Vitendo vya kinyuklia vilionekana vikiendelea, hatahivyo picha za Setlaiti katika kiwanda kikubwa cha kinyuklia cha taifa hilo wiki ilioipita zilionyesha kulikuwa na vitendo vilivyokuwa vikifanyika-zikidai kwamba huenda Korea kaskazini inatengeneza mionzi kuwa mafuta ya bomu.
Taifa hilo linadai kwamba limetenegeza bomu la kinyuklia ambalo linaweza kuingia katika kichwa cha silaha ya masafa marefu pamoja na kombora ambalo linaweza kufika Marekani
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni