Alhamisi, 9 Mei 2019

kingbees officialvideo usiniache




ngoma mpya toka kwa kingbees_tz plz lets support good music.

Mamia ya waombolezaji wamiminika kumuaga Mengi kijijini Machame leo

Maelfu ya waombolezaji wamehudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Usharika wa Moshi mjini wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kuhudhuria ibada hiyo, polisi walilazimika kufunga barabara zote ambazo zinaelekea kwenye kanisa hilo.
Safu ya waombolezaji imeongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la nchi hiyo Job Ndugai.
Mapema asubuhi saa tatu kanisa lilikuwa limejaa, na nje pia kulikuwa pamefurika. Baadhi ya waombolezaji walipata nafasi ya kuaga mwili ndani ya kanisa lakini ilifika mahala hatua hiyo ilisitishwa ili ibada na hotuba zitolewe.
Mwili ulitolewa kanisani kwa safari ya mwisho ya makaburini saa tisa na nusu. Na shughuli za mazishi zilikamilika saa 11 na nusu.

Familia yatoa neno

Familia
Image captionMke wa Mengi Jacquiline akiwa pamoja na watoto katika ibada ya mwisho ya mazishi ya mume wake
Mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu Mengi, Abdiel, amesema kwa niaba ya familia wanashukuru na wameguswa na upendo waliooneshwa.
"Sisi kama familia tumeguswa sana na upendo ambao umeoneshwa kwa baba yetu. Mengi mazuri kuhusu mzee wetu mmeyasema. Mapenzi yao yamemgusa mzee wetu, hili ni uthibitisho kuwa muda na nguvu zake ambazo aliziwekeza kwa watu hawa hazikupotea bure. "
Abdiel amemzungumzia baba yake kuwa ni mtu ambaye alipenda kufanya mambo mengi na kujaribu na alikuwa na mipaka yake pia.
Mazishi ya Mfanyibiashara maarufu wa Tanzania Reginald Abraham Mengi
"Lakini hakuwa na mpaka kwenye kupambana na umasikini. Alikuwa na mtoto wa masikini lakini hakuna aliyeweza kumzuia kupambana na umasikini na kujikwamua. Pia hakukubali mpaka wa kuambiwa yeye kama mwekezaji mzawa basi hawezi fanya hili ama lile nchini. Hilo alilipinga kwa nguvu zote."
Jamaa waliyojawa na majonzi
Marehemu Mengi ameacha mjane, ambaye ni mlimbwende maarufu nchini humo Jacqueline Ntuyabaliwe na watoto wanne.
Umauti ulimfika usiku wa Jumatano ya wiki iliyopita jijini Dubai, Falme za Kiarabu ambapo alienda kwa ajili ya matibabu.

Mengi ni nani?

mENGIHaki miliki ya pichaIPP
Mengi alizaliwa wilayani Machame, Kilimanjaro, Tanzania mwaka 1942, akiwa mmoja wa watoto saba wa Bw Abhraham Mengi na Bi Ndeekyo Mengi.
"Familia yetu ilikuwa masikini sana, kila siku ilikuwa ni vita ya kupambana na umasikini. Tulimiliki sio zaidi ya ekari moja tukiishi kwenye vibanda vya udongo tukichanganyika na ng'ombe wachache na kuku. Ninaporudisha fikra na kutazama nyuma ni vigumu napatwa na ugumu wa kufikiri namna tulivyoweza kuishi katika hali ile," alipata kusema kwenye uhai wake.
Alianza safari yake kielimu shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School. Kwa ufadhili wa Chama cha Ushirika kilichokuwa na nguvu ya kifedha ushawishi KNCU Mengi alisomeshwa masomo yake ya shahada ya kwanza ya uhasibu nchini Uingereza.
Baada ya masomo ughaibuni, Mengi alirudi Tanzania 1971 na kuajiriwa na kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ( sasa PricewaterhouseCooper) mpaka mwaka 1989 alipoamua kujikita kwenye ujasiriamali.
Baada ya kuachana na ajira, Mengi aliiboresha kampuni yake ya Industrial Projects Promotion Limited na baadae kufahamika zaidi kama IPP Limited.
Kupitia IPP Limited Mengi alaianzinza kampuni mbalimbali na kufanya biashara kadha wa kadha kuanzia uzalishaji wa sabuni, soda, maji ya kunywa, madini, mafuta, gesi asilia na kilimo.
Hata hivyo, umaarufu mkubwa wa Mengi ni kutokana na kumiliki vyombo vya habari, kuanzia magazeti, vituo vya runinga na redio.
Mwaka 2014, jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes lilikadiria utajiri wa Mengi kuwa unafikia dola milioni 560.
    WAOMBOLEZAJI

    Noti ya $50 ya Australia ina makosa ya herufi katika neno uwajibikaji

    50 dollar billHaki miliki ya pichaRESERVE BANK OF AUSTRALIA
    Image captionKumbuka kuangalia maandishi kwenye pesa zako
    Noti mpya nchini Australia ya $50 imechapishwa ikiwa na makosa ya herufi, ambayo inatazamwa kuwa aibu.
    Benki ya akiba ya Australia (RBA) imeandika neno "responsibility" yaani jukumu hivi - "responsibilty" - katika mamilioni ya noti hizo mpya za rangi ya njano.
    Imethibitisha kosa hilo la herufi leo na kueleza kwamba litasahihishwa katika noti zitakazochapishwa katika siku zijazo.
    Lakini kwa sasa, takriban noti milioni 46 zinatumika nchini
    Zilichapishwa mwishoni mwa mwaka jana na zinamuonyesha Edith Cowan, mbunge wa kwanza mwanamke nchini Australia.
    Kinachoonekana kama nyasi nyuma ya bega la Bi Cowan, ni maandishi madogo mno - ya nukuu ya hotuba yake ya kwanza bungeni.
    Presentational white space
    "Ni jukumu kubwa kuwa mwanamke wa kipekee hapa, na nataka nisisitize haja iliopo kwa wanawake wengine kuwepo hapa," ni maneno yalioandikwa na kuregelewa mara kadhaa kwa hati ndogo mno katika noti hiyo.
    Na neno jukumu kwa kizungu 'responsibility', limechapishwa mara zote bila ya herufi 'i' - na kuandikwa "responsibilty
    Imechukua zaidi ya miezi 6 kutambua makosa hayo ya herufi.
    50 dollar note with magnifying glassHaki miliki ya pichaRESERVE BANK OF AUSTRALIA
    Noti hiyo ya $50 ndiyo inayotumika sana Australia, na imesambaa pakubwa.
    Wakati noti hiyo mpya ilipochapishwa mnamo Oktoba, iliundwa kwa vigezo vya kiusalama kuzuia kuighushi
    Na kama basi unajiuliza iwapo noti hiyo inatumika - ndio, noti hiyo yenye makosa ya herufi inatumika kama sarafu ya nchini humo

    Korea Kaskazini yafanya tena jaribio la makombora yake

    Korea Kaskazini Kim Jong akiongoza zoezi la kufanyia majaribio makombora ya nchi hiyo wiki iliyopitaHaki miliki ya pichaEPA/KCNA
    Image captionKorea Kaskazini Kim Jong akiongoza zoezi la kufanyia majaribio makombora ya nchi hiyo wiki iliyopita
    Korea Kaskazini imerusha makombora mawili ya masfa mafupi, limesema jeshi la Korea Kusini.
    Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Sino-ri lililopo Kaskazini Magharibi mwa mji mkuu wa Pyongyang.
    Hatua hiyo inakuja wakati balozi wa Marekani anaehudumu huko Korea kazkazini Steve Beigun anazuru Korea kusini kutafuta vipi mazungumzo hayo yanaweza kuanzishwa upya.
    Wachambuzi wanatafsiri kitendo hicho ni kutokana na kutoridhika kwa utawala wa Pyongyang na kuvunjika kwa mwendelezo wa mazungumzo yao na Marekani yaliyokuwa yafanyike mwezi February huko mjinii Hanoi.
    Mwezi uliyopita Korea Kaskazini ilisema kuwa imefanyia majaribio silaha yenye kombora kali , ikiwa ni mara ya kwanza tangu mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Kim Jong un kugonga mwamba.
    Tunafahamu nini kuhusu hatua hiyo?
    Makombora mawili ya masafa mafupi yalirushwasaa kumi unusu skwa saa za huko, ilisema taarifa ya pamoja ya wakuu wa kijeshi kutoka taifa jirani la Korea Kusini.
    Uchunguzi wa kina unafanywa kwa ushirikiano na maafisa wa upelelezi wa Marekani, iliongeza taarifa hiyo.
    Rais wa Korea kusini Moon Jae-in amemuonya kiongozi wa Korea kaskazini kutoondelea na tabia yake ya kufanya majaribio ya kufyatua makombora.
    Amesema kwamba hatua hiyo itatetelesha uhusiano wao na Marekani na vilevile utawala huo wa Seoul.
    Location of Sino-ri base
    Mzozo wa nyuklia unatokana na nini?
    Hali ya taharuki imezuka kati ya Korea kaskazini na Marekani baada ya Washington kusisitiza kuwa Pyongyang ikomeshe mpango wake wa nyuklia.
    Kiongozi wa Korea kazkazini Kim Jong-un anataka vikwazo dhidi ya nchi yake viondolewe na mazoezi ya kijeshi kati ya Marekani na Korea kusini yasitishwe.
    Jumamosi iliyopita Korea Kaskazini ilithibitisha kuwa rais Kim Jong-un ameongoza mwenyewe shughuli ya kufanyia majaribio makombora kadhaa ya masafa ya kadri na yale ya masafa ya mbali.
    MakomboraHaki miliki ya pichaAFP/KCNA VIA KNS
    "Makombora kadhaa ya masafa mafupi" pia yalirushwa kutoka rasi ya Hodo hadi bahari ya Japan.
    Mwaka uliopita , kiongozi huyo wa Korea alisema kuwa atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia na kwamba hatofanyia majaribio makombora ya masafa marefu huku uwezo wa Kinyuklia wa Pyonyang ukibainika.
    Vitendo vya kinyuklia vilionekana vikiendelea, hatahivyo picha za Setlaiti katika kiwanda kikubwa cha kinyuklia cha taifa hilo wiki ilioipita zilionyesha kulikuwa na vitendo vilivyokuwa vikifanyika-zikidai kwamba huenda Korea kaskazini inatengeneza mionzi kuwa mafuta ya bomu.
    Taifa hilo linadai kwamba limetenegeza bomu la kinyuklia ambalo linaweza kuingia katika kichwa cha silaha ya masafa marefu pamoja na kombora ambalo linaweza kufika Marekani