Baraza la jeshi linaloongoza nchini Sudan linasisitiza kuwa Sheria ya dini ya Kiislam itasalia kuwa muongozo wa sheria mpya za nchi hiyo.
Viongozi wa waandamanaji wamewasilisha orodha ya mapendekezo wanayotaka yazingatiwe na serikali ya mpito baada ya rais Omar al-Bashir kuondolewa madarakani mwezi Aprili.
Lakini baraza hilo lenye wanachama 10 limesema kuwa "lina mashaka" na mapendekezo hayo- Luteni-Jenerali Shamseddine Kabbashi, ambaye ni msemaji wa baraza la mpito la jeshi lililochukua uongozi baada ya Bw. Bashir kutimuliwa uongozini, amaewaambia wanahabari kuwa wamekubaliana na mapendekezo yote yaliyotolewa na waandamanaji.
Hata hivyo ameongeza kuwa mapendekezo hayo, "hayakugusia chanzo cha sheria, na kwamba sheria ya dini ya Kiislam itasalia kuwa muongozo wa kutunga sheria mpya".
Katiba ya sasa ya Sudan inasema kuwa sheria ya kiislam ndio muongozo wa maadili ya taifa.
Hata hivyo chini ya utawala wa Bw. Bashir sheria hiyo ilitumika kibaguzi na wanaharakati walikuwa wakisema inawalenga wanawake.
Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za wanawake yalisema maelfu ya wanawake waliadhibiwa kwa kupigwa kwa ''kuinesha tabia mbaya'', kwamujibu wa shirika la habari la AFP.
Luteni Jenerali Kabbashi alisema kuna baadhi ya masuala yenye utata katika mapendekezo hayo.
Waandamanaji walikua wamependekeza kuwa uwezo wa kutangaza hali ya hatari ipewe mawaziri mawaziri hata hivyo TMC inaamini kuwa hilo ni jukumu la serikali halisi ambayo bado haijabuniwa.
Pia walikua wamependekeza kipindi cha mpito ambacho kiitadumu kwa miaka minne, huku jeshi likishikilia kuwa muda huo unstahili kuwa miaka miwili.
Ili kupata ufumbuzi wa mkwamo uliyopo kuhusiana na suala hilo Luteni-Jenerali Kabbashi amesema, wanatafakari uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi katika kipindi cha miezi sita.
- Amjad Farid, msemaji wa mojawapo wa makundi makubwa ya waandamanaji, chama cha wataalamu wa Sudan (SPA), amesema kwanza watafanya uchunguzi wao "na baadae tutatangaza msimamo wao baadae".
Awali afisa wa ngazi ya juu katika baraza la jeshi aliiambia BBC kuwa hawatakubali kubuniwa kwa serikali ya mpito ya kirai -tamko ambalo limekosolewa vikali.
Makundi ya waandamanaji yameendelea kupiga kambi mbele ya makao makuu ya jeshi mjini Khartoum, wakishinikiza kubuniwa kwa utawala wa kirai waandamanaji wamekuwa ''kimya kuhusu sheria ya Kiislam'
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni