Jumapili, 5 Mei 2019

Ni kwanini si rahisi kumpata mtu kama Mengi nchini Tanzania?

Imekuwa ni wiki ya majonzi kwa Watanzania na majirani zake baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Reginald Mengi tarehe 2 Mei, 2019 kilichotokea Dubai katika Falme za Kiarabu.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka miaka 77. Wengi wanamkumbuka kwa kuwa mfanyabiashara mahiri na mmiliki wa kampuni ya IPP Limited na IPP Institute of Technology and Innovation. Huku Watanzania wakijianda kumpumzisha, baadhi wanajiuliza iwapo Tanzania itampata mtu atakayeweza kuziba pengo aliloliacha.
Lakini Mengi alikuwa ni mtu wa aina gani?


Reginald Mengi ametajwa na wengi kuwa alikuwa ni mtu aliyetafuta maslahi si yake tu bali kwa jamii nzima ya Watanzania



Mengi amekuwa akijitoa katika kusaidia wasionacho na wenye uhitaji kwenye jamii ikiwemo walemavu wa ngozi na kugharamia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo nchini India. Kila mwaka Dr. Reginald Mengi alijiwekea utaratibu wa mwaka mpya unapoingia alikuwa akiandaa chakula cha mchana na kula na wenye ulemavu wa kila aina nchini Tanzania, kitu ambacho hakitasahaulika miongoni mwa Watanzania:
Ukarimu kwa watu wenye ulemavu ni miongoni mwa sifa zinazoendelea kuenziwa kwa Dr.Mengi
Japo alikuwa ni mwanachama wa chama tawala cha CCM Bwana Mengi aliweza kuwa na maelewano mazuri na watu wa tabaka mbali mbali wakiwemo wanasiasa wa kada mbali mbali na hivyo kuvuka mipaka ya uhasama wa kisiasa baina ya kambi mbali mbali za kisiasa nchini Tanzania.
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto kabwe anaamini bwana Regnald Mengi alikuwa na mchango mkubwa katika kukuza demokrasia nchini Tanzania
Image captionKiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto kabwe anaamini bwana Regnald Mengi alikuwa na mchango mkubwa katika kukuza demokrasia nchini Tanzania
''Mengi kama alivyosema yeye alikuwa mwanachama wa CCM , lakini kusema ukweli ni mtu ambaye amekuwa akiunga mkono pia upinzani ili kuwe na upinzani imara nchini, amewahi kutoa msaada wa kufanya juhudi halali kabisa za kisasa kwa upinzani. Ni mtu ambaye alipoona kuna jambo halali la kushughulikiwa kwa ajili ya manufaa nchini alikuwa anazungumza moja kw amoja na wa pande zote kuhakikisha jambo hilo linatendeka, alikuwa na mchango mkubwa kabisa katika kuhakikisha kunakuwa na demokrasia nchini''. Ameiambia BBC, kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Zitto Kabwe.
Si Tanzania pekee alikofahamika na kupendwa na watu mbali mbali waliotambua kazi zake na mchango wake katika maendeleo ya nchi yake na maisha ya Watanzania kwa ujumla.
Hii imedhihirika baada ya kifo chake kwani watu kutoka mataifa na tabaka mbali mbali wamemwagia sifa kwenye mitandao ya kijamii hususan kupitia Twitter kupitia Hastag Mengi ilianzishwa:
Mengi hakuwa mtu wakukata tamaa
Waliomfahamu Bwana Reginald Mengi wakati wa uhai wake wanasema hakuwa mtu mwenye kukata tamaa.
Wakati mambo yalipaoonekana kwa wengine kuwa ni magumu, alitumia fursa hiyo kujitafutia suluhu ya kibinafsi na pia kutoa suluhu kwa matatizo ya jamii nzima ya Watanzania.
Mfano Mwaka wakati Tanzania ilipokumbwa na uhaba wa bidhaa karibu zote baina ya miaka ya 1983 1984, alihangaika kupata kalamu ya kuandikia na hatimae akaweza kuandika kitabu alichokiita - I Can, I Must, I Will- kinachomaanisha -Ninaweza, Lazima , nitaweza.
Bwana Mengi aliamsha ari yake ya ujasiriamali na akaamua kuanza kuagiza bidhaa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Miongoni mwa bidhaa za kwanza alizoziagiza Mengi ni Kalamu za wino kutoka Mombasa Kenya.
"Wakati mizigo ulipowasili sikujua niiuweke wapi. Kwa hiyo , mahala pasuri pa kuiweka palikuw ani chumbani kwanguna ilikuwa ni katika chumba kileambako nilianza kupanga kalamu zangu ," aliliambia jarida la Forbes Africa toleo la Julai 2014.
Alinyimwa mkopo wa $4,000 kutoka kwa benki ya taifa ya biashara (NBC) inayomilikiwana , lakini hakukata tamaa na akaamua kuzungumza na wafanyabiashara wenzake nchini Kenya na baadaye akapata fedha hizo.
Wakati serikali ilipokabiliana na kuwakamata wafanyabiashara ikiwashutumua kwa kuuza bidhaa muhimu kiholela, ndipo Bwana Mengi alipoamua kutoacha biashara daima na kuamua kuzipanua biashara zake katika maeneo mengine, ikiwawemo kuanzisha kiwanda cha vinywaji vya Coca-Cola mjini Moshi, kilichoitwa Bonite Bottlers Mwaka 1987.
Aliuza dawa za kusafisha viatu zilizotengenezwa kwa mkaa na mafuta, na vipodozi vya kusugua mwili mwili asilia vitokanavyo na matope ya baharini
Aliendelea kutengeneza kila kitu alichokiweza kuanzia: karatasi za usafi wa maliwato, sabuni, kemikali za usafi, vitanda nadawa za meno.

Image captionSalim Kikeke mwandishi wa BBC, alimfahamu Bwana mengi kama mtu ambaye hakujikweza japo alikuwa na umaarufu na utajiri mkubwa
Na hatimae akaamua kujitosa katika uwekezaji katika tasnia ya habari na kumiliki vyombo mbali mbali vya habari yakiwemo magazeti, redio na televisheni ambavyo vilimpatia umaarufu mkubwa.
Licha ya mazingira magumu ya uhuru wa habari nchini Tanzania, Mengi aliweza kujitosa katika tasnia ya habari na kuanzisha vituo mbali mbali vya televisheni, redio na magazeti ambavyo vimetoa mchango mkubwa wa ajira na kukuza vipaji vya kwa waandishi wa habari nchini Tanzania.
''Kwa kweli naweza kusema hapa nilipofika sasa ni kutokana na mengi, nimepitia mikononi mwake nilipokuwa nafanya kazi katika kituo chake cha televisheni cha ITV, na hata nilipokuja huku Uingereza aliniruhusu na baadaye aliniuliza iwapo nitarudi kufanya kazi Tanzania kufanya kazi ITV, nikamwambia bado ninafanya kazi hapa, lakini akashauri kuwa iwapo ningependa kuendelea kufanya kazi BBC ni sawa tu niendelee. Kwa kawaida si waajiri wengi watakaokuambia uendelee kufanya kazi ulipo huku wakiona una kipaji na unawaponyoka'' Alisema mwandishi wa Televisheni ya Kiswahili ya BBC - Swahili Dira TV, Salim kikeke alipokuwa akimkumbuka Bwana Mengi.
Salim aliongeza kuwa: '' Kitu kingine nilichojifunza kwake ni kwamba japo alikuwa ni mtu tajiri mwenye mafanikio na umaarufu lakini hakujikweza alikuwa ni mtu wa watu, hilo nimejifunza kutoka kwake''
Hadi mauti yake Bwana Mengi alikuwa muanzilishi na mwenyekiti mtendaji wa IPP Limited pamoja na IPP Institute of Technology and Innovation


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni