Jumapili, 5 Mei 2019

Steinunn Gunnsteinsdóttir: Mwanzilishi wa kampuni ya utengenezaji ngozi ya samaki

Steinunn Gunnsteinsdóttir anakiri kuwa iliichukua familia majaribio ya mara kadhaa kuweza kutengeneza ngozi kutokana na samaki.
"Mara 200 ya kwanza tulitengeneza supu ya samaki iliyokuwa na harufu kali," alisema.
Bi Gunnsteinsdóttir ni meneja wa mauzo wa kampuni ya Atlantic Leather kutoka Iceland ambayo inajihusisha na biashara ya bidhaa za samaki Barani Ulaya
Tangu mwaka 1994 kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza ngozi kutokana na samaki wa aina kadhaa kama vile salmon, perch, na cod.
Shughuli ya kutengeneza ngozi hiyo huchukua kati ya wiki mbili hadi tatu, na wafanyikazi 19 wanaweza kutengeneza karibu tani moja ya ngozi ya samaki kwa mwezi.
"Harufu ya samaki hubadilika katika awamu ya kwanza ya utengenezaji wake, na baadaye hubadilika na kunukia kama ngozi ya kawaida," anaongeza Bi Gunnsteinsdóttir.
Ngozi ya samaki inaendelea kupata umarufu wa kutengenezewa vibeti vya wanawakeHaki miliki ya pichaFAO/LUIS TATO
Image captionNgozi ya samaki inaendelea kupata umarufu wa kutengenezewa vibeti vya wanawake
Kampuni hiyo inapata malighafi yake kutoka Iceland, Norway na visiwa vya Faroe.
Tofauti na utengenezaji wa ngozi inayotokana na ng'ombe ambayo inasemekana kuwa hatari kwa mazingira utengenezaji wa ngozi wa samaki ni salama kwa mazingira.
Atlantic Leather pia inatumia 'dye' ya kawaida na ile isiyo na athari kwa mazingira kutengeneza ngozi kutokana na samaki
Bei ya ngozi inategemea aina ya samaki kwa mfano ngozi inayotokana na samaki aina ya salmon inauzwa kwa dola $12.
Kipochi kilichotengenezwa kutokan na ngozi ya samakiHaki miliki ya pichaCAMILLE THIEBAUT
Image captionKipochi kilichotengenezwa kutokan na ngozi ya samaki
Bidhaa zao zinaagizwa sana na kampuni maarufu za mitindo kama vile Jimmy Choo, Dior na Ferragamo, na Bi Gunnsteinsdóttir anasema kumekuwa na dhana kuwa ngozi inayotokana na samaki sio dhabiti na inaweza kuchanika kwa urahisi.
"Ngozi ya samaki ni imara mara kumi zaidi ya ngozi ya ng'ombe" anasema.
"Hii ni kwasababu ngozi ya samaki inapitana pitana bada ya kwenda juu na chini... hali ambayo inaifanya kuwa thabiti zaidi hasa kwa utengenezaji wa mishipi, viatu na vibeti vya wanawake."
Japo ngozi inayotokana na samaki inachangia chini ya 1% ya mauzo ya ngozi duniani, shirika la chakula na kilimo duniani (FAO) kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa zinahamasisha ukuzaji zaidi wa ngozi hiyo ili kuwaongezea kipato wafanyibiashara wa smaki duniani.
Wafanyikazi wa kiwanda cha ngozi cha Victorian Foods nchini KenyaHaki miliki ya pichaFAO/LUIS TATO
Image captionWafanyikazi wa kiwanda cha ngozi cha Victorian Foods nchini Kenya
"Tunadhani ngozi ya samaki ndio njia bora ya kuimarisha maisha ya watu bila kuhatarisha usalama wa chakula ," anasema Jackie Alder,ambaye ni afisa wa kitengo cha uvuvi wa shirika la FAO
Ongezeko la upatikanaji wa ngozi ya samaki litapunguza uhitaji wa ngozi ya nyoka na wanyama wengine ambao wakabiliwa na hatari ya kuangamia duniani
Utumiaji wa ngozi ya samaki pia siku zijazo huenda ikapunguza uhitaji wa ngozi ya ng'ombe ambayo mfumo wake wa utengenezaji sio salama kwa mazingira.
Viwanda vya utengenezaji ngozi inayotokana na ng'ombe imehusishwa moja kwa moja na ongezeko la ulaji nyma.
Kiwango cha sasa cha ulaji nyama na ngozi ya ng'ombe kinakadiriwa kuchangia tani milioni ya uchafuzi wa mazingira kila mwaka.Tangu mwaka 2005, makundi ya kampuni zinazojihusisha na utengenezaji ngozi ambayo wanachama wake ni pamoja naAdidas, Nike na Primark -yanasema yamekuwa yakishinikiza umuhimu wa kutunza mazingira.
Mkurugenzi wa Victorian Foods James AmbaniHaki miliki ya pichaFAO/LUIS TATO
Image captionVictorian Foods inapata malighafi yake kutoka kwa wavuvi 300
Kampuni ya Kenya inayofahamika kama Victorian Foods pia kwa ushirikiano na Jackie Alder na kundi lake wanatumia samaki kutoka ziwa Turkana kutengeneza ngozi.
Afisaa mkuu mtendaji wa Victorian Foods' James Ambani anasema katika kipindi cha miaka mitatu cha utendakazi wake kampuni hiyo sasa inatengeza kilo 400 za ngozi kwa wiki ambayo inauzwa kwa dola tano kwa mraba.
Kampuni hiyo imewaajiri wanawake 10 na imekuwa ikiwapa mafunzo makundi ya watu wanaojihusisha na biashara ya utengenezaji ngozi inayotokana na samaki.
Ngozi ya samaki huenda ikapunguza uhitaji wa ngozi ya mambaHaki miliki ya pichaFAO/LUIS TATO
Image captionNgozi ya samaki huenda ikapunguza uhitaji wa ngozi ya mamba
Mwanamitindo wa mavazi mzaliwa wa Kenya Deepa Dosaja hivi karibuni alitumia ngozi ya samaki kutengeneza vibeti vya wanawake..
"Hii ni fasheni ya hali ya juu na inapendeza sana - najivunia kuimarisha taaluma yangu," anasema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni