Golikipa wa kimataifa raia wa Uhispania David de Gea, 28, amepewa wiki moja ili kuamua mustakabali wake na klabu yake ya Manchester United. (Sun)
Barcelona wametangaza dau nono na la kushtukiza la pauni milioni 70 ili kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Mfaransa Alexandre Lacazette, 27. (Sunday Express)
Manchester United wanaweza wakapewa nafasi ya kumsajili kipa wa Real Madrid Keylor Navas, 32, katika kipindi hiki ambacho hawana uhakika endapo De Gea atasalia klabuni hapo. (Telegraph)
Chelsea wametakiwa kuheshimu makubaliano waliyoingia na na mshambuliaji wao Eden Hazard ya kuwa ili ajiunge na Real Madrid, alitakiwa kusalia klabuni hapo msimu huu na pale utakapoisha ataruhusiwa kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania. (Sun)
Manchester City wanajipanga kuchuana na Barcelona katika mbio za kumsajili beki na nahodha kinda wa Ajax Matthijs de Ligt, 19, mwenye thamani ya pauni milioni 65. (Star)
Kiungo wa Manchester United Juan Mata yawezekana akarejea Uhispania msimu ujao - huku klabu ya Athletic Bilbao ikimuwania kiungo huyo mwenye miaka 31 kwa udi na uvmba. (Mirror)
Zinedine Zidane amekataa kuhusishwa na uvumi juu ya uhamisho wa wa kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26, kwenda Real Madrid. (Manchester Evening News)
Pogba ameambiwa kuwa hatapata nafasi nyengine tena ya kuhamia Madrid endapo hatafanya hivyo mwishoni mwa msimu huu. (Sun)
Beki wa Atlanta United Florentin Pogba, 28, ambaye ni kaka wa Paul, anaamin: "kuna kitu kitatokea majira haya ya kiangazi" na amekataa kusema iwapo mdogo wake hatohamia moja wapo ya klabu kubwa za Uhispania Real Madrid ama Barcelona for his sibling. (AS, via Calciomercato)
Kocha aliyetimuliwa kazi na Manchester United Jose Mourinho, 56, amepatiwa ofa ya kuifundisha klabu ya AS Roma kwa miaka mitatu, lakini atajiunga na klabu hiyu endapo watafuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya. (L'Equipe, via Mail on Sunday)
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameahidiwa na uongozi wa klabu hiyo kuwa atawezeshwa ili afanye usajili mkubwa hivi karibuni. (Sun)
Tetesi kali za Jumamaosi
Barcelona inaanda dau la £30m kwa Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Willian, 30. (Sun)
Manchester City imefanya mkutano na wazazi wa beki wa Benfica joao Felix 19 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Manchester United na Liverpool. (Record, via Express)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameanzisha harakati zake za kumsajili mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 22. (L'Equipe, via Mirror)
Chelsea itaanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 23, kuhusu mkataba mpya . (Sun)
Mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Bayern Munich, atauzwa kwa dau la £36m na Real Madrid mwisho wa msimu huu na klabu za Manchester United na Chelsea huenda zina hamu ya kumsajili mchezaji huyo.27. (Marca, via Express)
Mchezaji wa Paris St-Germain aliyesainiwa kwa rekodi ya dunia Neymar, 27, huenda akauzwa kwa dau la £145m mwisho wa msimu huu kutokana na sheria inayomzuia kuuzwa . (Mundo Deportivo, via Mirror)
Mkufunzi wa Tottenham Mauuricio Pochettino ameonya Tottenham kwamba atalazimika kufanya mabadiliko yenye 'uchungu' mkubwa ili kuimarisha klabu hiyo kuwa katika kiwango cha uwanja mpya. (London Evening Standard)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni