Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya Mtandao wa Kijamii wa WhatsApp, PCK ambaye ni raia wa nchini Burundi alisema kuwa, kwa hivi sasa amehamia kwa Zari baada ya kuachana na Wema hivyo wakati ukifika ataweka wazi kila kitu.
Alitiririka kuwa, licha ya kuwa na mke wa ndoa, lakini pia Zari ni mtu wake na uhusiano wao una wiki mbili sasa na haoni ajabu au shida kuwa na mke wa ndoa na mpenzi wa pembeni kwa kuwa yeye siyo wa kwanza kufanya hivyo.
“Kwa sasa nimehamia kwa Zari ila siwezi kuweka wazi picha zangu na Zari, ila muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi maana itakuwa siyo siri tena. “Najua watu wengi hawaamini wanachokisikia, lakini ndiyo hivyo kwani Zari ninamfahamu tangu enzi za mumewe Ivan (marehemu Ssemwanga),” alisema PCK .
ATAJA SABABU YA KUACHANA NA WEMA
Akizidi kumwagika, PCK ambaye kwa siku za usoni amekuwa akirusha madongo kwa Wema kupitia Mtandao wa Instagram alisema aliamua kuachana na Wema kutokana na kwamba amekuwa akimtukana mkewe kila kukicha hivyo akaona isiwe tabu. “Wema anazingua sana, amekuwa akimtukana sana mke wangu kila siku kwenye simu, kitu ambacho sikufurahishwa nacho, nikaamua kukata naye mawasiliano tu maana niliona atavunja ndoa yangu,” alisema PCK.
HAPA INAKUWAJE?
Wakati PCK akikiri kuhamia kwa Zari, mwaka 2017 aliwahi kukiri kuwa kwenye uhusiano na mdogo wa mwanamama huyo aliyemtaja kwa jina la Asmah, jambo ambalo linazua mshangao na maswali kwa watu kuwa inakuwaje anachanganya mtu na mdogo wake?
ALIMWINGIZA WEMA MATATANI
Mwaka jana, PCK alimwingiza matatani Wema ambaye walikuwa naye kwenye uhusiano wa kimapenzi baada ya kuvuja kwa video na picha zao za faragha mitandaoni huku akimtapeli mamilioni ya fedha na kutokomea.
Tangu kutokea kwa ishu hiyo, Wema hajawahi kurudi kwenye ubora wake kutokana na maumivu aliyoyapata huku akikabiliana na kesi ya picha chafu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. Wakati mambo yakiwa hivyo kwa upande wa Wema mwanaume huyo aliyekuwa na makazi jijini Dar alikimbilia nchini kwao, Burundi hivyo hadi sasa anasakwa na Polisi nchini.
PCK WANTED BONGO
Msanii huyo, mbali na kusakwa kwa picha hizo chafu alizopiga na Wema pia Jeshi la Polisi nchini linamsaka kwa kumtapeli kigogo ambaye ni Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina kapuni).
PCK anahusishwa pia na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kuwafanyia ‘ushenzi’ mastaa kibao wa kike. Kutokana na CV (wasifu) huo wa PCK, baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili juu ya ukaribu wake na Zari, walimtaka mwanamama huyo kuwa makini na mwanaume huyo.
MBALI NA WEMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni