Jumapili, 3 Februari 2019

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 02.02.2019: Solskjaer, Hudson-Odoi, Willian, Bakayoko


Manchester United watampatia kazi meneja wao wa sasa Ole Gunnar Solskjaer akifanikiwa kushinda Paris St-Germain katika mchuano wao wa ligi ya mabingwa. (Sun)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ameelezea kutoridhishwa kwake na usimamizi wa klabu hiyo baada ya kushindwa kusajili wachezaji wapya kwa misimu miwili mfululizo. (Mirror    Chelsea watakabiliana na Bayern Munich katika uhamisho wa mshambuliaji Callum Hudson-Odoi, baada ya klabu hiyo ya Bundesliga kushindwa kumsajili nyota huyo wa miaka. (Sun)

Hudson-OdoiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHudson-Odoi, wa kati

Winga Willian, 30 wa Chelsea na Brazil, anataka kusaini mkataba wa miaka mitatu, lakini kuna tetesi amepewa mkataba wa mwaka mmoja. (Sport Witness)
Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini alitaka kumsaini mchezaji wa zamani wa Cardiff, Gary Medel mwezi Januari lakini juhudi zake zilitibuka baada ya Besiktas kuitisha ada ya uhamisho. (Talksport)
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti anaamini Arsenal "walimlaghai" winga wa Croatia Ivan Perisic, 29, katika pendekezo la uhamisho wa Januari. (Rai Sport via Independent)

Tiemoue BakayokoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTiemoue Bakayoko, kushoto

Kiungo wa kati wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko, 24, ambaye yuko AC Milan kwa mkopo kutoka Chelsea, amesema angependelea kusalia katika klabu huyo ya Italia. (Corriere dello Sport via Four Four Two)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anahofia mlinzi wake Joe Gomez,21 huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji. (Liverpool Echo)
Newcastle wanajianda kutangaza kuondoka kwa kocha wao wa zamani Peter Beardsley ambaye alikua mkufunzi wa timu ya wachezaji wa chini ya miaka -23. (Mail)

Mada zinazoh

Manchester United hawajashindwa hata mechi moja chini ya uongozi wa Ole Gunnar Solskjaer

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni