Jumapili, 3 Februari 2019

Maurizio Sarri: Hazard na Higuain ni hatari sana

     Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri anasema kuwa Gonzalo Higuain na Eden Hazard ni moto wa kuotea mbali baada ya wawili hao kufunga magoli mawili kila mmoja katika mechi ya ushindi dhidi ya Huddersfield hatua ilioirejesha Chelsea katika nafasi yake ya nne.
Lilikuwa bao la kwanza la Higuain tangu alipojiunga na Chelsea kwa mkopo kutoka Juventus katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
''Higuian anazidi kuimarika'' , alisema Sarri.  Hakuwa katika kiwango chake cha kawaida alipowasili, kwa sababu alikuwa na jeraha la mgongo kwa hivyo akacheza kwa dakika chache''.
''Ni mchezaji mzuri. Mbali na magoli hayo ni mzuri kushirikiana karibu na Eden''.
Raia huyo wa Argentina alifunga goli la kwanza kunako dakika 16 katika mechi hiyo iliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge.
N'Golo Kante alimpatia pasi murua akaweza kuichenga safu ya ulinzi na kufunga. Kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika Elias Kachunga alimuangusha Cesar Azpilicueta na refa Paul Tierney akampatia penalti, licha ya fauli hiyo kuonekana kufanyika nje ya eneo hatari.
Higuain na Eden Hazard
Hazard alifunga penalti hiyo na kufunga bao lake la kwanza la ligi tangu Dusemba 26.
Raia huyo wa Ubelgiji alifanya mambo kuwa 3-0 kunako dakika ya 66, alipomzunguka kipa Jonas Lossl na kufunga kutoka pembeni.
Na dakika tatu baadaye Higuain alipata bao lake la pili baada ya kuukunja mkwaju wake karibu na lango la wapinzani .
David Luiz alifunga bao la tano katika dakika za mwisho baada ya kufunga kichwa kikali kutoka kwa kona iliomfanya Kachunga kujifunga.
Ushindi huo ulisitisha wiki mbaya ya Sarri kufuatia matokeo mabaya ya kichapo cha 4-0 dhidi ya Bournemouth.
Chelsea sasa iko nafasi ya nne , ikiwa na pointi tatu juu ya Arsenal ambao wanacheza dhidi ya Man City siku ya Jumapili.
Lakini ni kipigo cha 11 kati ya mechi 12 kwa Huddersfield ambao wanasalia chini ya jedwali la ligi .Higuain akifunga mojawapo ya magoli yake mawili dhidi ya Huddersfield

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni