Jumapili, 3 Februari 2019

Tuna El-Gebel: Kaburi lenye miili hamsini iliohifadhiwa lapatikana Minya Misri

  Miili 50 iliokuwa imehifadhiwa na inayodaiwa kutoka katika enzi za Ptolemaic (miaka ya 305-30BC imepatikana na mwanakiolojia, kulingana na wizara ya vitu vya zamani.
Miili hiyo ambayo 12 kati yao walikuwa watoto ilipatikana katika makaburi manne yenye kina cha urefu wa mita tisa katika eneo la Tuna El-gebel huko Minya kusini mwa mji mkuu wa Cairo.
Baadhi ya miili hiyo ilikuwa imefungwa ndani ya kitambaa huku mingine ikiwa ndani ya majeneza ya mawe na yale ya mbao.  Hawajatambulika ni watu gani , maafisa wanasema lakini huenda walishikilia nyadhfa za juu.

Eeneo la Tuna El-GebelHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEneo la Tuna El-Gebe llililopo Minya, kusini mwa mji wa Cairo
Miili iliofungwa ndani ya kitambaa ikiwa na vipande vipande vya michoro.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionVipande vipande vya mawe vilvyochorwa vilikuwa ndani ya miili hiyo.
Miongoni mwao ni fuvu hili la kichwa liliofungwa ndani ya kitambaaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiongoni mwao ni fuvu hili la kichwa liliofungwa ndani ya kitambaa
Watoto ni miongoni mwa miii iliopatikana huko MinyaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatoto ni miongoni mwa miii iliopatikana
Baadhi ya miili hiyo ilipatikana ndani ya majeneza ya maweHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya miili hiyo ilipatikana ndani ya majeneza ya mawe
Wizara ya vitu vya zamani nchini Misri inasema kuwa miili hiyo huenda inatoka kwa watu wa familia zinazojiwezaHaki miliki ya pichaAFP
Image caption
Wizara ya vitu vya zamani nchini Misri inasema kuwa miili hiyo huenda inatoka kwa watu wa familia zinazojiweza     Egyptian mummies

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni