Jumanne, 7 Mei 2019

Ajali ya ndege Moscow: Watu 41 wauawa baada ya ndege ya Aeroflot kuanguka

Watu arubaini na moja wameuawa baada ya ndege ya Urusi kutua kwa dharura na kulipuka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow.
Video katika mitandoa ya kijamii zinaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura na kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea moto.
Watoto wawili na mhudumu mmoja ni miongoni mwa waliofariki kwa mujibu wa vyombo vya habari 
Shahidi mmoja amesema ilikuwa ni "miujiza" kwamba kuna aliyenusurika mkasa huo wa ndege, iliyokuwa imebeba abiria 73 na maafisa wataano wa ndege.
"Watu 37 wamenusurika - Abiria 33 na maafisa wanne wa ndege hiyo," amesema afisa wa kamati ya uchunguzi, Yelena Markovskaya.
Watu watano wamo hospitalini.
Aeroflot, shirika la ndege la kitaifa Urusi limesema ndege hiyo ililazimika kurudi katika uwanja wa ndege " kutokana na sababu za kiufundi", lakini halikufafanua zaidi.
Ndege nyingine zimelazimika kuelekezwa katika viwanja vingine wa ndege nchini.
Russian plane catches fire in MoscowHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMoshi mweusi umeenea utoka kwenye ndege inayoteketea katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo
Russian plane catches fire in MoscowHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege ndiyo ilikuwa imeanza kuondoka kutoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo ilipoanza kuteketea
Ndege ilifanyika nini?
Ndege hiyo aina ya Sukhoi Superjet-100, iliondoka uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mwendo wa saa 18:02 kwa saa ya huko kutoka eneo la Murmansk.
Maafisa wa ndege wakatoa tahadhari ya wasiwasi wakati kulishuhudiwa " hitilafu" muda mfupi baada ya ndege kuondoka.
Baada ya kutuwa kwa dharurua katika uwanja huo wa ndege , injini za ndege hiyo ziliwaka moto katika njia kuu wa ndege, Aeroflot limesema katika taarifa.
Maafisa hao wa ndege "walijitahidi kadri ya uwezo wao kuwaokoa abiria ," waliofanikiwa kutolewa katika muda wa sekundi 55, shirika hilo la ndege limeeleza.
Russian plane flight map
Aeroflot limechapisha orodha ya walionusurika mkasa huo (kirusi) ambao kufikia sasa wametambuliwa, likiongeza kwamba litaendelea kutoa taarifa kadri wanavyozipokea.
Taarifa pia zinaashiria kwamba ndege hiyo haikufanikiwa katika jaribio la kwanza la kutuwa kwa dharura.
Kaimu Gavana wa mji eneo hilo la Murmansk, Andrey Chibis inaarifiwa amesema familia za waliofariki katika mkasa huo watalipwa $15,300 kola mmoja, huku waathirikwa watatibiwa katika hospitali na watapewa $7,650 kila mmoja.
Sheremetyevo airportHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAmbulensi zinasubiri katika mojawapo wa kiingoilio kikuu katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo
Manusura walitoroka vipi?
Mikhail Savchenko anadai alikuwa ndani ya ndege hiyo wakati ilipolipuka moto lakini alifanikiwa "kuruka nje".
Alituma video ya abiria waliokuwa wakitoroka kutoka kwenye ndege hiyo iliyokuwa inawaka moto na kuandika ujumbe: "'niko sawa, niko hai na salama."
Mojawapo ya manusura, Dmitry Khlebushkin, amesema anawashuru sana wahudumu wa ndege hiyo.

    "Shukran sana kwa wahudumu, nimenusurika," amewaambia waandishi habari.
    Kristian Kostov, aliyekuwa mshindani katika mashindano ya Ulaya, Eurovision, raia wa Bulgaria ameandika katika mtandao wa kijamii kuhusu alichoshuhudia.
    Alieleza kwamba watu katika uwanja wa ndege walishutushwa baada ya kuona ndege hiyo ikiteketea moto na akaeleza kwamba ndege nyingine sasa zimeshindwa kuondoka.
    Uchunguzi umeidhinishwa sasa kufahamu zaidi kuhusu mkasa huo taarifa zinasema.
    Rais wa Urusi Vladimir Putin inaarifiwa tayari keshapewa taarifa na ameeleza masikitiko yake kwa familia za waathiriwa.
    Eneo hilo la Murmansk limetangaza siku tatu za maombolezi

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni