Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi umewasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere Dar es salaam kutoka Dubai ambapo alifikwa na umauti Jumatano iliyopita.
Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo amesema mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Tanzania utahifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo baada ya kuwasili.
Siku ya Jumanne, Siku ya Jumatano Mei 8, 2019 mwili utasafirishwa kwenda Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika siku ya Alhamisi Mei 9, 2019.
"Baada ya mwili kuwasili Machame ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania la Kisereni,"
Umauti ulimfika akiwa na umri wa miaka 77, huku akicha mke na watoto wanne.
Mengi alizaliwa wilayani Machame, Kilimanjaro, Tanzania mwaka 1942, akiwa mmoja wa watoto saba wa Bw Abhraham Mengi na Bi Ndeekyo Mengi.
"Familia yetu ilikuwa masikini sana, kila siku ilikuwa ni vita ya kupambana na umasikini. Tulimiliki sio zaidi ya ekari moja tukiishi kwenye vibanda vya udongo tukichanganyika na ng'ombe wachache na kuku. Ninaporudisha fikra na kutazama nyuma ni vigumu napatwa na ugumu wa kufikiri namna tulivyoweza kuishi katika hali ile," alipata kusema kwenye uhai wake.
Alianza safari yake kielimu shule katika shule ya msingi Kisereny Village Bush School, kisha akajiunga Nkuu District School, kisha Siha Middle School, na baadaye Old Moshi Secondary School.
Kwa ufadhili wa Chama cha Ushirika kilichokuwa na nguvu ya kifedha ushawishi KNCU Mengi alisomeshwa masomo yake ya shahada ya kwanza ya uhasibu nchini Uingereza.
Baada ya masomo ughaibuni, Mengi alirudi Tanzania 1971 na kuajiriwa na kampuni ya Cooper and Lybrand Tanzania ( sasa Prince water house Cooper) mpaka mwaka 1989 alipoamua kujikita kwenye ujasiriamali. ataagwa katika viwanja vya Karimje
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni