HUZUNI na majonzi makubwa! Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, marehemu Dkt Reginald Mengi amejikuta katika hali mbaya ya kushindwa kujizuia baada ya mwili wa mumewe kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo Jumatatu, Mei 6, ukitokea Dubai ambako umauti ulimkuta.
Baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakimfariji na kumpa pole, lakini kutokana na hali ya kibinadamu alijikuta akimwaga machozi jambo ambalo liliibua hisia kubwa miongoni mwa waombolezaji waliokuwepo uwanjani hapo.
Mwili wa marehemu Dkt Mengi umepelekwa katika Hospitali ya Lugalo na ambao utaagwa kesho, Jumanne katika Ukumbi wa Karimjee, Posta Jijini Dar Es Salaam na Jumatano utasafirishwa kwa ndege kwnda kwao Machame ambako utazikwa Alhamisi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni